Unayempenda Hakupendi? Sababu Zote Hizi Hapa.

Kuanzisha mahusiano na mwanamke au mwanaume unayempenda ni jambo rahisi sana endapo kila mmoja ataridhishwa na tabia au mwonekano wa mwenzake. Lakini huwa ni jambo gumu pale mmoja wapo anakosa vigezo vya kumnasa mwingine.

Unayempenda Hakupendi sababu ni hizi

Ukiwa unataka kumnasa mwanamke au mwanaume hadi aseme umenibamba unatakiwa utumie muda na wala sio jambo la kufumba na kufumbua. Tafiti zinaonesha watu wengi waliodumu kwenye mahusiano yao ni wale walioanza kuwa na ukaribu na baadae wakaanza mahusiano.

Hii maana yake ni kwamba ukianza kuwa karibu na mwanamke au mwanaume unapata kujua uzuri wake siku akiwa amependeza na siku akiwa hajapendeza, siku akiwa na furaha na siku akiwa na hasira. Baada ya kufahamu na kuzoea mwenendo wa mwenzako moyo automatically unaanza aidha kumkubali au kumkataa.

SABABU 6 ZINAZOFANYA UKATALIWE NA MTU UNAYETAKA KUANZA NAE MAHUSIANO

1. VIGEZO ANAVYOTAKA

Unaweza kuwa ni mrembo au handsome lakin ukakataliwa na mtu unayemtaka kwasababu tu haujakizi vigezo anavyotaka. Mfano yeye anahitaji mtu mrefu lakini ww ni mfupi, anahitaji mweupe lakin ww ni mweusi.Hapo unakuwa haujakidhi vigezo richa ya kuwa na ukaribu nae au mwonekano mzuri.

2. MAHUSIANO YAKE YA SASA

Unaweza kuwa na vigezo vyote anavyotaka lakini atakukataa kwasababu yupo kwenye mahusiano ambayo kwa muda huo ndo yako motomoto. Yani hapo tunasema ni sawa na mchezo wa mpira wa miguu upo kipindi cha pili umeshapigwa goli 3 kwa sifuri sasa unatakiwa uchomoe magoli 3 na uongeze.

Sio kazi ndogo na hata kama utafanikiwa kumpata basi kutakuwa na sababu ya muda mfupi tu kama vile anahitaji pesa ya kununua simu mpya na akishaipata kwako ataaza vituko muachane.

3. HISTORIA YA MAHUSIANO YAKO

Unaweza kukataliwa kwasababu ya historia ya mahusiano yako sio nzuri. Mfano labda uliwahi kuwa na mahusiano na mtu mwenye UKIMWI, au watu waliowahi kuwa na mahusiano na wewe wanakusema vibaya. Jitahidi sana kuwa na sifa nzuri kwenye mahusiano ili usiache doa.

4. KAZI YAKO

Unaweza kataliwa na mtu kwasababu tu ya kazi yako ya kutafuta kipato. Sitaki kusema Mengi maana hapa wengi sana ndo wanapolalamika.

5. WATU WAKO WA KARIBU

Unaweza kataliwa na mtu umpendae kwasababu ya watu wako wa karibu kuwa labda wana tabia za hovyo HIVYO na wewe kuonekana ni miongoni mwao. Jiepusha na watu wenye sifa mbaya usijekosa mtu umpendae.

6. UCHANGAMFU WAKO

Tabia yako ya kuongea na kucheka na kila mtu wa jinsia tofauti na yako inaweza kuwa sababu ya wew kukataliwa kwani mtu unayemtaka anahofia kuumizwa na hao watu unaocheka nao kila siku. 

Mwingne anaweza jua kuwa ni WAPENZI wako. Kuna ule msemo unasema Sitakubali mpenzi wangu awe na marafiki wa karibu kwasababu hata Mimi na yeye tulianza kwa kuwa marafiki. Kwahyo safari moja huzusha nyingine.


WE UNAFIKIRI SABABU NYINGNE NI IPI?

Post a Comment

0 Comments